Mwigulu awaonya watumishi wazembe

WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameonya watumishi wezi na wazembe. Dk Mwigulu alitoa onyo hilo aliposimama kusikiliza kero za wafanyabiashara katika Soko la Machinga jijini Dodoma. “Mtanuna mpaka mpasuke, sitacheka na wavivu, sitacheka na wezi, sitacheka na wadokozi, sitacheka na mzembe na Katiba imetoa mamlaka hayo ya udhibiti, usimamizi wa shughuli za serikali na usimamizi wa maelekezo ya Rais Samia, wasome Katiba wajue,” alisema.

Dk Mwigulu aliagiza kuwekwe mazingira mazuri ya ufanyaji biashara katika soko hilo ikiwemo miundombinu ya barabara, maji na umeme. “Nimeshaelekeza wahusika wa wizara pamoja na mkoa watapita waangalie, lakini mmeongelea kuongeza taa na pia watapita kuja kuangalia na jenereta watapita kuangalia aina ya jenereta ili waweke muweze kufanya biashara vizuri,” alisema.

Dk Mwigulu ameutaka uongozi wa Mkoa wa Dodoma uweke mazingira bora ya soko kwa kumtafuta mkandarasi atakaeweka maeneo mazuri ya ufanyiaji biashara yanayohamishika. “RAS (Katibu Tawala wa Mkoa), Mkuu wa Mkoa tafuteni mtaalamu anayeweza kuweka mpangilio kwenye hii eneo ambacho hakina nguzo nyingi, kiwekwe kitu ambacho kinaweza kuhamishika hata kama maeneo haya sio ya soko la kudumu,” alisema.

Ameongeza : “Utaratibu huu wa kuwa kila mmoja anaweka mfuko wa sandarusi, miamvuli, mwingine maboksi kwenye majiji na halmashauri hapana, tuendelee kubuni vitu nadhifu, Rais Samia kuanzia bajeti hii inayokuja anaongeza asilimia tano, kwenye ile 4,4,2 kutakuwa na asilimia 15, asilimia 5 ni kwa ajili ya miundombinu.”

Dk Mwigulu ameziagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita ichunguze tuhuma za viongozi waliotafuta mafundi wa kujenga ofisi ya veta wilayani Nyang’hwale kwa lengo la kujipatia fedha. SOMA: Dk Mwigulu ataka ushirikiano wa kikanda mapambano dhidi ya saratani

“Wanatafuta mafundi wao, wanatafuta wakandarasi wao ili wagawane fedha, sasa Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Geita nenda kachunguze pale Nyang’hwale nipate taarifa ili nione wale wanaoitanguliza fedha ya umma kule mbele ili wakachukulie mbele,” alisema.

Dk Mwigulu ameagiza mamlaka zinazohusika na ajira kumfukuza kazi muuguzi aliyemfanyia upasuaji wa tumbo mgonjwa kwenye kochi nyumbani kwake mkoani Tabora. “Unafanya majaribio kwenye maisha ya mtu, maisha ya binadamu unayafanyia majaribio,

Rais kajenga hospitali kila kona tuna hospitali za wilaya, tuna hospitali za rufaa, kuna vituo vya afya sasa hivi vinahadhi kama hospitali ya wilaya unaenda kumfanyia mgonjwa chumbani nyumbani kwako, kwenye kochi upasuaji, huyu ni mmoja ya watu wanaokiuka maadili ya taaluma zao,” alisema.

Ameongeza : “Huyu si wa kuhamishwa, afukuzwe kazi mara moja na akishafukuzwa apelekwe kwenye mkono wa sheria na wale wanaotoa vibali vya kitaaluma wamnyang’anye hicho kibali, kidogo kidogo tutaelewana tu, Mkuu wa Mkoa wa Tabora mkamateni mfukuzeni kazi aondolewe hiyo hadhi lakini pia afikishwe kwenye mkono wa sheria”.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button