Mwigulu atoa agizo usafiri mwendokasi

SERIKALI imetoa siku 10 kwa watendaji wa taasisi zinazohusika na usafiri wa mwendokasi Dar es Salaam wainishe maeneo ya kufanyiwa kazi haraka.

Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo alipozungumza na wakazi wa Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara katika kata ya Mbezi wilayani Ubungo mkoani humo.

Dk Mwigulu alikuwa katika ziara ya siku moja kukagua miundombinu iliyoharibiwa katika vurugu zilizotokea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu.

SOMA: Dk. Mwigulu akagua uharibifu wa vurugu

“Wizara ya Ujenzi, TANROADS, DART, UDART, OWM-TAMISEMI, TANESCO na wadau wengine, kaeni kuanzia leo, husisheni mabenki rejesheni intaneti, umeme, mageti ya kukatia tiketi ili turejeshe hali ya mpito wakati tukitafuta suluhisho la kudumu,” alisema.

Dk Mwigulu alisema anaungana na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapa pole walioathirika na vurugu za Oktoba 29.

“Tuangalie upya hatua zetu tunazozichukua. Rais Samia Suluhu Hassan aliunda Tume ili kuliangalia jambo hili, ninawaomba tumuunge mkono Mheshimiwa Rais na wajumbe wa tume iliyoundwa ili kuchunguza undani tukio la vurugu zilizotokea, tujue namna lilivyofanyika na hatua stahiki zitakazochukuliwa,” alisema.

Dk Mwigulu alisema Rais Samia ameelekeza kusiwe na maadhimisho ya sherehe za Uhuru Desemba 9, mwaka huu na badala yake fedha ambazo zingetumika kwenye sherehe hizo zitumike kurekebisha miundombinu iliyoharibika katika vurugu za Oktoba 29.

Ameelekeza viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na sekta zinazohusika wakae na kuratibu fedha hizo ili jambo hilo lifanyike haraka kutekeleza agizo la Rais Samia.

Kwa upande wake, Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Riziki Shemdoe alisema Sh bilioni 12.5 zinahitajika kurejesha miundombinu ya mabasi ya mwendokasi Dar es Salaam katika hali ya kawaida.

Shemdoe alisema katika barabara ya mwendokasi kutoka Kariakoo kwenda Kimara vituo 20 vimeharibiwa kwa kuchomwa moto au kupigwa mawe.

Alisema maeneo yaliyoharibika sana ni mifumo ya umeme, mifumo ya kukusanyia nauli, vioo vya vituo na maeneo mwingine ya miundombinu hiyo.

Msamaha taasisi za dini
Dk Mwigulu alisema Rais Samia amesamehe taasisi za kidini zenye changamoto na kuielekeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifungulie Kanisa la Ufufuo na Uzima na taasisi nyingine za kidini.

Alisema kanisa hilo lipewe miezi sita ya uangalizi katika kuzingatia miiko, masharti na sheria za uendeshwaji wake.

“Waziri wa Mambo ya Ndani, baada ya hapa fuatilia utaratibu mzuri ziandikie upya taasisi za kidini, miiko yao na masharti ya uandikishaji na zile ambazo zilikuwa na shida ziweke kwenye uangalizi wa miezi sita, ipo taasisi ya Ufufuo na Uzima nenda kaifungulie. Ifungulie, wape masharti ya uangalizi ndani ya miezi sita. Ziandikie taasisi zote za kidini kuzikumbusha miiko na mipaka ya ufanyaji kazi, sawa sawa na sheria na Katiba ya nchi yetu,” alisema Dk Mwigulu.

Sambamba na hilo ameelekeza kurekebishwa kwa sharti linalotaka kufungiwa kwa nyumba ya ibada endapo
atakosea kiongozi, akisisitiza kuwa anayekosea ndiye aadhibiwe bila kuathiri waumini kufanya ibada.

“Akikosea Shehe, usiadhibiwe msikiti na akikosea Askofu, wasinyimwe waumini kufanya ibada kwani ibada ni ushirika kati ya mwanadamu na Mungu wake na siyo yeye na askofu au shehe,” alisema Dk Mwigulu.

Madhara ya Oktoba 29
Dk Mwigulu alisema madhara ya Oktoba 29 ni pamoja na wananchi kupoteza maisha wakiwemo wasio kuwa na hatia yoyote. Kuharibiwa ofisi za serikali za kata zaidi ya 700, kuharibiwa pamoja na mabasi ya mwendokasi, nyumba binafsi, magari binafsi, vituo vya polisi, mahakama na vituo vya mafuta pamoja na biashara za watu binafsi.

“Maeneo yanayoguswa ni yale nyeti kabisa katika nchi ambayo binadamu wa kawaida hauwazi kuyagusa ndio yanayolengwa. Unatengenezwa ugomvi unaohusisha dini zetu huyo mtu anaitakia mema nchi yetu, ni familia
gani katika nchi yetu ambao wao kwenye ukoo wao wapo kwenye dini moja pekee?”alisema.

Dk Mwigulu alisema jambo hilo ni kubwa ndio maana Rais Samia ameunda tume ya uchunguzi.

“Hili sio jambo dogo, na kwenu nyie ambao hamjafuatilia mambo ya nchi za Afrika mnaweza kuliona jambo rahisi tu limetokea Tanzania na wengine wanaweza wakalizungushia kwenye kamviringo kadogo ka uchaguzi  na wengine wanaweza kuzungushia kwenye kamviringo kadogo ka vyama vya siasa,” alisema.

Aliwataka vijana wa Kitanzania kuilinda nchi yao kwa sababu Mungu aliwapa nchi nzuri ya Tanzania yenye
utajiri mwingi na kwamba Tanzania si mali ya serikali wala ya vyama vya siasa bali ni mali ya Watanzania wote.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button