Mwigulu atoa maelekezo hoja za wabunge miradi ya maendeleo

DODOMA; SERIKALI imesema imefuatilia kwa makini mijadala ya wabunge na kuwa hoja zao zimeonesha wazi kuunga mkono juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Februari 6, 2026 kwenye hotuba yake ya kuahirisha shughuli za Bunge la 13 Mkutano wa Pili ulioanza Januari 27, 2026.
“Waheshimiwa wabunge wameeleza matarajio yao ya kuona miradi hiyo, hususan ya maji, nishati, barabara na miundombinu mingine, inakamilika kwa haraka ili wananchi waanze kunufaika kikamilifu.
“Tayari nimewaelekeza Mawaziri wa Fedha, Ujenzi, Maji, Nishati pamoja na TAMISEMI kuandaa mchanganuo wa kina wa miradi yote iliyoidhinishwa na inayoendelea kutekelezwa kwa kusuasua au kusimama.
“Mchanganuo huo pia uhusishe miradi iliyosainiwa na haijaanza kutekelezwa, na ile ambayo hati zake zimewasilishwa na malipo hayajafanyika ili kuweka mkakati madhubuti wa kukamilisha malipo na hatimaye kuharakisha utekelezaji wake kwa wakati.
“Ninatoa maelekezo mahsusi kwa waheshimiwa mawaziri husika kuhakikisha zoezi hili linakamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti, ili hoja za waheshimiwa wabunge zichukuliwe hatua kwa vitendo na miradi ikamilike kwa viwango vinavyotarajiwa,” amesema Waziri Mkuu.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com