Mwinyi aagiza balozi kukibidhaisha

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka Watanzania kwa ujumla wao kushirikiana katika kukikuza na kukieneza Kiswahili ndani na nje ya nchi na kufungua fursa za ajira.

Pia, ameziagiza Balozi za Tanzania zilizoko katika nchi mbalimbali duniani kuanzisha vituo vya lugha ya Kiswahili na utamaduni wake kwa lengo la kujitangaza na kueneza Kiswahili nje ya nchi.

Dk Mwinyi aliyasema hayo Unguja, Zanzibar jana wakati akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema hatua hizo kwa kiasi kikubwa zitaifanya lugha ya Kiswahili kujitosheleza na kuongezeka kwa matumizi yake na kutumiwa na kuzungumzwa na watu wengi duniani.

Alizipongeza baadhi ya Balozi za Tanzania ambazo tayari zimefungua vituo vya kufundishia Kiswahili ikiwemo Korea Kusini, Italia, Falme za Kiarabu, Uholanzi, Zimbabwe, Ufaransa, Cuba, Nigeria na Sudan.

“Natoa pongezi za pekee kwa ubalozi wa Korea Kusini kwa kuanzisha mafunzo ya utamaduni wa Mswahili yanayohusisha mambo tofauti ikiwemo vyakula, mavazi, ngoma na lugha,” alisema.

Alisema ni wakati sasa wa balozi za Tanzania kuona haja ya kuanzisha vituo vya lugha ya Kiswahili na utamaduni wake kwa lengo la kujitangaza na kueneza Kiswahili nje ya nchi.

Aidha, alizipongeza wizara zote za Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa ubunifu ulioongeza hasama ya maadhimisho hayo ya Kiswahili ikiwemo kuanzishwa kwa mbio zilizoitwa Swahili marathoni zilizofanyika Arusha kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kukuza utalii nchini.

Akizungumzia maadhimisho hayo ya Kiswahili alisema kupewa siku yake maalumu ni heshima kubwa kwa Tanzania hivyo ina wajibu wa kuwapongeza wote waliotoa rai ya kuanzishwa kwa siku hiyo adhimu inayoipa nguvu lugha ya Kiswahili kutambuliwa duniani kote.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana alisema lugha ya Kiswahili inatumika na wananchi wasiopungua milioni 500 duniani na inazidi kuongezeka matumizi yake kwa kasi.

Alisema Watanzania wanapaswa kujivunia kupata maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kwa kuwa sasa lugha hiyo inazidi kupaa ulimwenguni.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kathleen D. Holloway
Kathleen D. Holloway
2 months ago

I make $100h while I’m traveling the world. Last week I worked by my laptop in Rome, Monti Carlo and finally Paris…This week I’m back in the USA. All I do are easy tasks from this one cool site. check it out,
AND GOOD LUCK.:)
.
.
.
HERE====)>>>>>> https://fastinccome.blogspot.com/

BerniceNickell
BerniceNickell
2 months ago

This year do not worry about money you can start a new Business and do an online job I have started a new Business and I am making over $84, 8254 per month I was started with 25 persons company now I have make a company of 200 peoples you can start a Business with a company of 10 to 50 peoples or join an online job.

For more info visit on this web Site. . . . . . . . .>>> http://www.Richcash1.com

Last edited 2 months ago by BerniceNickell
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x