Zanzibar, Oman kuendelea kushirikiana

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Serikali ya Oman na kupongeza uhusiano mwema wa kindugu na kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Oman.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 09 Oktoba 2025, alipokutana na Waziri wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman, Sheikh Salim bin Mohammed Al Mahrouqi, aliyefuatana na Balozi Mdogo wa Oman anayefanya kazi zake Zanzibar, Said Salim Al Sinawi, pamoja na ujumbe kutoka Wizara hiyo ya Oman.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi amesisitiza dhamira ya Serikali ya Zanzibar kuendeleza uhusiano huo wa kihistoria kwa manufaa ya pande zote mbili, hususan katika maeneo ya utalii, utamaduni na uhifadhi wa urithi wa kihistoria.

Kwa upande wake, Waziri Mahrouqi amemshukuru Rais Dk Mwinyi kwa ukarimu wake na kueleza dhamira ya Serikali ya Oman kuendeleza ushirikiano uliopo, hususan katika programu ya ukarabati wa majengo ya kihistoria yanayofadhiliwa na Oman.SOMA: Tuache chokochoko tudumishe amani

Akiwa Zanzibar, Waziri Mahrouqi, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,  Mudrick Ramadhan Soraga, ametembelea majengo mbalimbali yanayofadhiliwa na Serikali ya Oman, yakiwemo Beit al Ajaib, Mtoni Palace, Kibweni Palace pamoja na majengo mengine yaliyomo ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button