ZSSF yatakiwa kusukuma miradi ya maendeleo

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefungua Soko la Mbogamboga la Mombasa Mjini Unguja na kuagiza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuongeza bidii katika miradi ya maendeleo ikiwemo kuanzisha teksi za baharini, basi na treni za umeme ili kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara.

Ameyasema hayo katika hafla iliyofanyika Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kama sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema katika soko hilo kipaumbele cha kwanza kiwe ni wale waliohamishwa. Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ukiwemo ujenzi na uboreshaji wa masoko, stendi za mabasi kwa usafiri wa umma pamoja na barabara kuu za mijini na vijijini.

Amesema hatua hiyo itaifungua Zanzibar kiuchumi na kuiwezesha kupiga hatua zaidi za maendeleo. “Tunapozungumza haya, watu wanadhani kama hadithi zisizotekelezeka, nawaagiza ZSSF pamoja na kazi nyingi nilizowapa, mfikirie kuwekeza kwenye mradi wa teksi za baharini na treni za umeme kama nilivyoahidi kwenye kampeni zangu, nataka kabla sijamaliza muda wangu niwe nimekamilisha hayo,” alisema.

Amesema serikali inapohamisha wafanyabiashara kutoka katika masoko yao kupisha matengenezo, inalenga kuwawekea mazingira mazuri kwa shughuli zao. Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, atahakikisha wanapatiwa mikopo nafuu kujiendeleza na kukuza mitaji yao.

Amepongeza juhudi za Kampuni ya Rans Limited iliyojenga soko hilo kwa kulijenga katika viwango vya juu akisema hali hiyo inatoa matumaini ya kampuni za wazawa kuaminiwa katika miradi mikubwa ya maendeleo.  Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Juma Malik Akil amesema ZSSF imeongeza mapato yake mara nne zaidi.

Akil amesema mapato hayo yameupa uhimilivu mfuko huo na utaweza kulipa mafao kwa wananchi watakaostaafu kwa miaka 50 ijayo bila shaka. “Mfuko huu umeweza kuongeza uwezo wake, ukwasi wake na kuwa na uwezo wa trilioni 1.36 ukikua zaidi ya mara nne kwa kulinganisha na miaka mitano iliyopita kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali kama vile kwenye soko la fedha Shilingi bilioni 800 na kuwekeza katika majengo na rasilimali mbalimbali ikiwemo soko lililofunguliwa,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF, Nassor Shaaban Ameir ambao ndio watekelezaji wa mradi huo, amesema Serikali ya Awamu ya Nane inalenga kubadili maisha kwa wananchi. Amesema wako tayari kutekeleza miradi yote iliyopo katika orodha yao ili kuleta maendeleo katika jamii. SOMA: Mwinyi Azindua Miradi ya Maendeleo Zanzibar

“Tuko mstari wa mbele kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo iko katika orodha yetu na tutaendelea hivyo ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi, ikiwa ndio dira na maono yako rais wetu unayotuelekeza na mradi wa mabasi ya umeme tutautekeleza hivi karibuni kama usafiri wa umma,” alisema.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button