Mwinyi: Hakuna atakayebaguliwa, wote ni wazanzibari

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kuwajali wananchi wote bila ubaguzi wa imani, asili au kundi la kijamii, akisisitiza kuwa “wote ni Wazanzibari.”
Akizungumza Oktoba 15, 2025, katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni, Dk. Mwinyi alikutana na wajane, wafuasi wa Rastafarian, pamoja na jamii za Wahindu na Ismailia, akiwaomba kura huku akiahidi maendeleo kwa wote. Alisema CCM imeendelea kuwa nguzo ya amani na mshikamano wa kitaifa, na kuwataka wananchi kuendeleza imani hiyo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29. SOMA: Wazanzibari wahimizwa kuchagua amani




