Mwisho wa tambo mashabiki Simba, Yanga leo

ILE siku, tarehe na mwezi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda soka nchini umefika.

Ni mchezo wa dadi ya Kariakoo Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SOMA: Gamond, Fadlu watambiana Kariakoo dabi

Advertisement

Mtananange huo ni mechi pekee ya ligi hiyo leo.

Simba ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 5 wakati Yanga ni ya 5 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 4.

Zifuatazo ni takwimu za michezo 5 ya Ligi Kuu iliyopita kati ya timu hizo:

Aprili 20, 2024: Yanga 2-1 Simba
Novemba 5,2023: Yanga 5-1 Simba
Aprili 16, 2023: Simba 2-0 Yanga
Oktoba 23, 2022: Yanga 1-1 Simba
Aprili 30, 2022: Simba 0-0 Yanga