Mzunguko wa 2 wavu taifa kuanza Sept 27

MZUNGUKO wa Pili wa Ligi ya Mpira wa Wavu Tanzania unatarajia kuanza Septemba 27 kwa michezo 14 kupigwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam.

Katika michezo ya Septemba 27 upande wa wanaume HighVoltage itashuka dimbani dhidi ya Faru wakati Tanzania Prisons itavaana na Chui huku The Capita wakicheza na Igombe.

SOMA: ‘Wekezeni michezo ya ufukweni’

Advertisement

Kwa wanawake Korosho Queens itakipiga dhidi ya Jeshi stars, JKT ikicheza na Mafinga Parish kisha baadae Jeshi stars itashuka dimbani tena dhidi ya Orkeeswa.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) Zacharia Bizmana, amesema maandalizi ya kiufundi yamekamilika.

“Kazi iliyosalia ni timu shiriki kujiandaa vizuri mzunguko wa pili wa ligi,” amesema Mkurugenzi huyo.

/* */