Nabi: Tunautaka ubingwa kesho

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mohamed Nasreeden Nabi, amesema anatamani kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji, ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nabi anasema anafahamu ugumu wa mchezo huo, lakini amewataka wachezaji wa timu hiyo kupambana, ili kupata alama tatu zitakaowafanya kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.

“Mchezo wa kesho ni muhimu kwetu, tunataka kushinda ili kumalizana na hesabu za ligi, tukicheza vizuri tutatengeneza morali kuelekea kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo Gallants,” alisema Nabi.

Advertisement

Kwa upande wake mshambualiji wa Yanga, Fiston Mayele anasema wanataka kumaliza kazi siku ya kesho.

“Sisi sio mashabiki furaha ya juzi imeshapita, kesho tuna jukumu la kuzitafuta alama tatu, ili  tuwe mabingwa,”  amesema Mayele.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji,   Kassim Liogope, amesema hawatokubali Yanga kutangaza ubingwa kupitia timu yake.

“Tutatumia mapungufu yao tuliyoyaona ili na sisi tuweze kupata matokeo, mchezo huu umekuja wakati ambao tuna uhitaji mkubwa na alama tatu,” amesema Liogope.

Ikiwa Yanga watashinda mchezo huo watajihakikishia ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara  kwa mara ya 29.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *