KENYA : BUNGE la Seneti nchini Kenya limeanza kusikiliza kesi inayomkabili Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Hapo jana, Jaji wa Mahakama Kuu Chacha Mwita amesema Mahakama ilitoa kibali kwa wabunge wa seneti kumuhoji Gachagua kwa mujibu wa katiba.
Hali hii inakuja wakati Naibu Rais akikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge wanaomtaka aondolewe madarakani kutokana na ukiukaji wa misingi ya uongozi.
Taarifa zinasema kuwa Gachagua alifika katika Bunge la Seneti leo asubuhi akiwa na mawakili wake waliojipanga kumtetea dhidi ya kesi yake huku matumaini ya kumaliza mzozo huo yakionekana kuwa chini.