DAR EA SALAAM: Kwa Watanzania wengi, msimu wa sikukuu ni wakati wa kusherehekea, kusafiri, na kujumuika na familia. Hata hivyo, kwa baadhi yao, mzigo wa kifedha unaotokana na gharama za usafiri unaweza kupunguza furaha zao wakati wa kipindi hiki muhimu.
Hapa ndipo Vodacom Tanzania ilipoingilia kati kupitia kampeni yake ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’, kuhakikisha kuwa sherehe za sikukuu zinawafikia watu wote, popote walipo.
Ikiwa na dhamira ya kusherehekea pamoja na wateja wake na kuhimiza urahisi wa miamala kupitia M-Pesa, Vodacom ilizindua kampeni hii maalum iliyowapatia maelfu ya Watanzania tabasamu la sikukuu. Kampeni hii ilifanyika msimu wa sikukuu za Krismasi, Mwaka Mpya, na kumalizika mwishoni mwa Januari 2025, ikiwawezesha wateja kurejeshewa nauli zao na punguzo la mafuta wanapofanya malipo yao kupitia M-Pesa Supa Mini App.
Zaidi ya kueneza furaha ya sikukuu, ‘Shangwe Popote’ iliimarisha dhamira ya Vodacom ya kuendeleza uchumi usiotegemea pesa taslimu. Kwa kuhamasisha matumizi ya M-Pesa, kampeni hii ilionesha urahisi na usalama wa malipo ya kidijitali, kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanafaidika na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi.
“Lengo letu lilikuwa kupunguza mzigo wa kifedha kwa wateja wetu na kuongeza furaha ya msimu wa sikukuu, huku tukiimarisha matumizi ya M-Pesa,” alisema Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania. “Kuona wateja wengi wakifaidika na malipo ya kidijitali ni uthibitisho kwamba miamala isiyotumia pesa taslimu ndiyo mustakabali wa kifedha. Tutaendelea na juhudi hizi ili kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa kila Mtanzania.”
Kupitia kampeni ya ‘Shangwe Popote’, Vodacom iliwarejeshea nauli wateja 194 waliokuwa wakisafiri kwa mabasi baada ya kununua tiketi kwa M-Pesa, ikiwapunguzia gharama za safari kwenda Moshi, Arusha, Morogoro, Mwanza na maeneo mengine. Pia, abiria wa treni ya SGR walifaidika, ambapo wateja 100 walipata tiketi za bure kwa safari kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, huku wateja wengine 120 wakifurahia punguzo la asilimia hadi 50 ya nauli zao.
Sherida Magomere, aliyekuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani, hakuamini bahati yake. “Sikutarajia kabisa kurejeshewa nauli yangu! Nilishangaa sana nilipoambiwa kuwa Vodacom inanirejeshea fedha. Hii ilifanya safari yangu kuwa ya kipekee zaidi, na hakika nitaendelea kutumia M-Pesa kufanya malipo yangu,” alisema.
Punguzo la mafuta pia lilikuwa sehemu muhimu ya kampeni hii, ambapo wateja 448 walipata punguzo maalum katika vituo vilivyochaguliwa vya mafuta jijini Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, na Mbeya. Aidha, wateja wa Bolt 374 walifaidika na marejesho ya asilimia 10 walipolipia kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu kupitia M-Pesa.
“Punguzo la mafuta limenisaidia sana. Mafuta ni kati ya gharama zangu kubwa, na kila shilingi ninayookoa inanisaidia kuongeza kipato. Niliweza kufanya safari nyingi zaidi bila kuhisi mzigo wa gharama za mafuta,” alisema Said Monyo, dereva wa bodaboda mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mwaka huu unapoanza, Vodacom Tanzania inasalia kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na kuhimiza malipo ya kidijitali kwa wote. Kampeni ya ‘Shangwe Popote’ ni mojawapo ya mipango mingi inayolenga kusaidia mabadiliko kutoka kwenye malipo ya kawaida ya pesa taslimu kwenda kwenye uchumi wa kidijitali.
Jambo moja liko wazi. Vodacom si tu mtandao wa mawasiliano ni mshirika wa wateja wake katika kusherehekea, kufanikisha malipo kwa urahisi, na kuwa sehemu ya maendeleo yao kiuchumi. Na kwa kampeni zaidi za kibunifu zinazoendelea, Watanzania wanaweza kutegemea fursa zaidi za kuokoa, kutengeneza kipato, na kusherehekea kwa raha na
uhakika.
What’s up everybody, here every one is sharing
such know-how, thus it’s good to read this weblog, and I used to pay a visit this website daily.
buy viagra online
payday loan
Hello would you mind letting me know which webhost
you’re working with? I’ve loaded your blog
in 3 different internet browsers and I must say this blog loads a
lot quicker then most. Can you recommend a good web hosting provider at a
reasonable price? Thanks, I appreciate it!
Touche. Soundd arguments. Keep upp the amazing spirit.