KLABU ya Namungo ya mkoani Lindi leo inashuka dimba la KMC Complex, Dar es Salaam ikiwa mgeni wa KMC katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
KMC ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 9 wakati Namungo ni ya 12 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 9 pia.
SOMA; KMC msimu ujao ligi kuu kama kawa
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliopigwa Oktoba 30, bingwa mtetezi Yanga imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kushinda mchezo wa 8 mfululizo ikiifunga Singida Black Stars kwa bao 1-0 lililofungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 67 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Kwa matokeo hayo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 24, haijapoteza wala kutoka sare mchezo wowote.