BAADA ya mechi 102 katika kipindi cha miaka minane, Gareth Southgate amejiuzulu kama kocha wa timu ya taifa ya England baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Hispania katika fainali ya Euro 2024 Julai 14, 2024.
Nafasi hiyo sasa iko wazi ikisubiri uteuzi wa kocha mpya.
Kumekuwa na kutajwa tajwa kwa baadhi ya makocha wanaoweza kuchukua mikoba hiyo ili kuirejesha England katika ubora iliyomaliza nao fainali ya Euro 2024.
Pamoja na wengine kocha wa England chini ya miaka 21, Lee Carsley anayeheshimika katika Shirikisho la Soka la England huenda akashangaza kwa kuteuliwa.
Carsley, mwenye umri wa miaka 50, alikuwa na mazungumzo kuhusu kuwa kocha Jamhuri ya Ireland mwaka jana lakini aliamua kubaki na England U21 kwa awamu nyingine.
Soma: Klopp kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu huu
Pep Guardiola: Kocha wa Manchester City amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kama kocha wa kimataifa wa siku za usoni na jukumu lake England linaweza kuwavutia mashabiki wengi wa nchi hiyo.
Guardiola ana mkataba na City hadi majira ya kiangazi 2025. Kazi hiyo inaweza kuwa chaguo lake lakini ingawa mshahara wake unaweza kuwa kikwazo kingine.
Mbali na Guardiola, Eddie Howe ni kocha mwingine wa England anayetajwa kwa kiasi kikubwa. Kocha wa Newcastle huyo mwenye umri wa miaka 46 ana mkataba wa muda mrefu hadi 2027, lakini inaweza kuwa ngumu kwa Howe kukataa fursa hiyo ikiwa England itamwita.
Jurgen Klopp ni kocha mwingine mwenye jina kubwa asiye na kazi.Klopp mwenye umri wa miaka 57 tayari anatajwa kwenda kuchukua nafasi Marekani na pia kama mrithi anayetarajiwa wa Julian Nagelsmann, iwapo ataondoka kuinoa Ujerumani.
Mbali na Klopp, Mauricio Pochettino ni kocha mwingine maarufu, anayependwa, wa kigeni asiye na kazi majira hayao ya kiangazi.
Pochettino pia anaaminika kuwa hana haja ya mapumziko yoyote katika kazi hiyo baada ya kuondoka Chelsea kwa makubaliano ya pande zote mwezi Mei.
Makocha wengine ambao huenda wakafikiriwa kuchukua mikoba England, kibarua ambacho huenda kikatanazwa muda si mrefuni pamoja na aliyekuwa kocha Brighton Graham Potter , kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel Meneja kocha wa Ipswich Kieran McKenna, kocha wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard, Kocha wa Middlesbrough, Michael Carrick, Kocha wa Celtic Brendan Rodgers na kovcha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.