Nani kuwafuata ‘Gen Z’ fainali Euro 2024?

BAADA ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania chenye vijana wengi ‘Gen Z’ kutinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya(EURO2024),leo Uholanzi na England zinakwaana kusaka atakayeshuka dimbani dhidi yao Julai 14.

Katika ushindi wa Hispania wa mabao 2-1, nyota wa Barcelona Lamine Yamal amevunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza nusu fainali ya Euro2024 akifunga bao maridadi dakika 21.

Ana umri wa miaka 16 na siku 362.

Winga wa kulia wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Barcelona, Lamine Yamal.

Nusu fainali hiyo ya pili leo itapigwa kwenye uwanja wa Signal Iduna ulipo jiji la Dortmund.

Mchezo huo unatarajiwa kuwawa kusisimua baada ya timu zote mbili kuonyesha ubora katika hatua za awali. Kutinga nusu fainali Uholanzi imeiondosha Türkiye kwa mabao 2-1 wakati England imeitoa Uswisi kwa bao1-0.

Timu ya Uholanzi imekuwa na matokeo mazuri, ikionyesha kiwango bora katika hatua za makundi na mechi za mtoano. Wachezaji wameonesha vipaji wakati muhimu.

Wachezaji muhimu wa kikosi hicho cha wadachi ni apmoja na Memphis Depay, Cody Gakpo, Frenkie de Jong, Virgil van Dijk. Uholanzi imeyonewlewa na Ronald Koeman imekuwa na  kawaida hutumia mfumo wa 4-3-3, ikitoa shinikizo kwa wapinzani kwa kucheza kwa mashambulizi ya haraka na kujilinda.

Kwa upande mwingine England pia imekuwa na kiwango cha kizuri kifika hatua ya nusu fainali. Ina mseto wa mbinu na wachezaji wenye vipaji vitu muhimu kwa mafanikio yao katika michuano.

Wachezaji muhimu katika kikosi cha England ni pamoja na Harry Kane, Bukayo Saka, Jude Bellingham, Declan Rice.

Soma zaidi: http://Ni Hispania au Ufaransa kutinga fainali EURO 2024?

Kikosi hicho chini ya Gareth Southgate kimekuwa na kawaida hutumia mfumo wa 4-2-3-1 kikiweka ulinzi, kucheza kwa ubunifu kwenye kiungo na uwezo wa kumalizia nafasi kwa usahihi.

Katika michezo 23 iliyopita kati timu hizo Uholanzi imeshinda 9, England 8 na zimetoka sare 6. Mechi ya leo inatarajiwa kuwa na vita eneo la Kiungo kati ya Frenkie de Jong wa Uholanzi na Jude Bellingham wa England.

Eneo la ulinzi kwa upande wa Uholanzi Virgil van Dijk anatarjiwa kuongoza safu huku England ikitarajiwa kuongozwa na Kyle Walker. Katika ushambuliaji, Memphis Depay atakuwa upande wa Uholanzi wakati Harry Kane ataongoza safu upande wa England.

 

Habari Zifananazo

Back to top button