NAOT yaridhishwa na utendaji MWAUWASA
TIMU ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (NAOT) imeridhishwa na utaalamu wa uondoshaji na jinsi ya kutibu majitaka unaofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).
–
Timu hiyo imetembelea eneo la mabwawa ya kutibu majitaka eneo la Butuja na kujionea hatua zinazopitiwa kutibu maji taka kuanzia hatua ya kwanza hadi hatua ya mwisho kabla ya kuruhusiwa kurudi ziwani.
–
Katika ziara hiyo wakaguzi hao waliambatana na wataalamu wa masuala ya usafi wa mazingira kutoka MWAUWASA pamoja na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Vitoria (LVBWB).
–
Awali kabla ya kutembelea eneo hilo la Butuja, timu hiyo ilipata fursa ya kukutana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Neli Msuya na kufanya utambulisho ofisini kwake. Imeandaliwa na Cyprian Magupa.