Nape: Mifumo ya Hospitali kuunganishwa

DAR ES SALAAM; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa hospitali zimekuwa na mifumo mingi na haisomani kiasi ambacho imechangia kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa wananchi.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya tatu ya kidijitali ya Afya na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili katika kampasi ya Mloganzanziala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo Waziri Nape amesema maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi ili kujadili namna TEHAMA inavyoweza kuboresha huduma za Afya.

“Tunataka kwa kupitia TEHAMA tuboreshe huduma hiyo ili mtu akienda kokote taarifa zake ziwepo,” amesema Waziri Nape.

Waziri Nape ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kufanya mifumo ya TEHAMA isomane ili kuweza kupunguza gharama kubwa ya matibabu kwa wananchi Pamoja na zile za uendeshaji.

Pa Waziri Nape amesema Kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano ambao ndo njia kuu ya kupeleka hizo taarifa na kuna mifumo kadhaa lazima itengenezwe ili taarifa ziwe pekee kwa kila mtu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
14 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions..
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x