Nchi 12 kusaka heshima michuano ya Gofu Arusha

ARUSHA: WACHEZAJI 220 kutoka nchi 12 Duniani wanashiriki mashindano ya gofu yanayofanyika katika Viwanja vya Kili gofu vilivyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Nchi hizo ni Tanzania Zimbabwe, ,Uganda,Afrika Kusini Ufaransa,Malawi,Kenya Rwanda,Nigeria Zambia Uholanzi na Cameroon

Mashindano hayo ya wazi yameandaliwa na chama cha Gofu Tanzania (TGU) na kudhaminiwa na benki ya NCBA.

Kati ya wachezaji hao 220, 54 ni wachezaji wa kulipwa kutoka maeneo mbalimbali.

Mashindano hayo ya wazi yamefunguliwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro ambaye amesema michezo ni uchumi na ajira na kusema yanakutanisha wachezaji kutoka ndani na nje ambao miongoni mwa ni wachezaji wa kulipwa.

“Haya ni mafaniko ya serikali katika kukuza michezo na kufanya wanamichezo wapate ajira kwani pia hapa kuna wachezaji wa kulipwa ambapo mshindi anapata milioni 10,” amesema Ndumbaro.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga amesema mashindano hayo ni ya siku nne na yatahusisha wachezaji wa kulipwa na wa ridhaa na yatamalizika Novemba 26.

Mkurugenzi mtendaji wa NCBA benki ,Claver Serumaga amesema wanafurahi kuwa sehemu ya waliofanikisha mashindano hayo ambayo yanakutanisha wachezaji mbalimbali na hii ni katika kuendeleza mchezo huu na kusema wataendelea kuunga mkono mchezo wa gofu.

Habari Zifananazo

Back to top button