Ndege mpya 5 ATCL kuwasili mwaka huu

NDEGE mpya 5 zilizonunuliwa na serikali zinatarajiwa kuwasili nchini mwaka huu 2023, ili kuendelea kuimarisha zaidi Shirika la Ndege nchini (ATCL).

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Januari 15 jijini Dodoma, akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni muendelezo wake wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuimarisha shirika hilo la ndege na kukuza utalii.

Msigwa amebainisha baadhi ya ndege hizo ambazo zitaanza kuwasili ni ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300, ambayo inatarajiwa kuingia nchini mwezi Machi na kufuatiwa na ndege mbili za abiria aina ya Boeing 737-9 Max, ambapo moja inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai na nyingine mwezi Oktoba.

Ndege nyingine ni kubwa ya abiria aina Boeing 787-8 Dreamliner, ambayo inatarajiwa kuingia nchini mwezi Novemba.

Msigwa amesema kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na watengenezaji wa ndege ya tano aina ya Bombardier Dash 8-Q400, ambayo ni ndege ya abiria, ili kujua itakuja linin a kuujulisha umma pindi watakapopata taarifa.

Habari Zifananazo

Back to top button