Ndumbaro: Somo la Kiswahili liwe lazima kwa wanafunzi wa kigeni

RUVUMA: Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ametoa rai kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuweka sharti la lazima kusoma somo la Kiswahili kwa wanafunzi ambao ni raia wa kigeni wanaojiunga na chuo hicho.

Ndumbaro amesema hayo mkoani Ruvuma wakati wa Mahafali ya 42 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea.

“Kiswahili ni bidhaa iliyo na wanunuzi wengi hivi sasa hivyo natoa rai kwenu uongozi wa chuo kuweka sharti la lazima la kusoma somo la Kiswahili kwa wanafunzi raia wa kigeni wanaojiunga na chuo”amesema

Advertisement

Aidha Dk Ndumbaro ametoa rai kwa chuo hicho kianzishe kozi za muda mfupi na mrefu katika upande wa burudani na michezo.

 

 

14 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *