Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2025 leo Novemba 5, 2025 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa NECTA Prof. Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa 937,581 sawa na asilimia 81.80 ya watahiniwa 1,146,164 wenye matokeo wamefaulu mtihani huo. (Picha na NECTA)