Wafanyabiashara wapunguziwe tozo

DAR –ES-SALAAM : KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amesema wafanyabiashara wengi wadogo wanakutana na changamoto kubwa ya kushindwa kulipa kodi kutokana na uwepo wa tozo nyingi zinazowakumba.

Akizungumza kuhusu uzoefu wake, changamoto zinazowakuta wafanyabiashara hao na mapendekezo ya kuboresha mifumo ya kodi, Beng’i Issa ametoa wito kwa Tume ya Maboresho ya Mifumo ya Kodi kuangalia kwa umakini na kuboresha njia bora ya ukusanyaji wa kodi, ili kuzingatia hali ya wafanyabiashara wadogo.

“Wafanyabiashara wadogo wanakutana na tozo nyingi za halmashauri ambazo zinawakwaza sana. Hizi tozo nyingi zinaathiri uwezo wao wa kulipa kodi na kudumisha biashara zao,” alisema Issa.

Advertisement

“Tunaomba Tume ya Maboresho ya Mifumo ya Kodi ione namna bora ya kusaidia wafanyabiashara hawa na kuwawezesha kulipa kodi kwa njia rahisi na ya haki.”

SOMA:  Mapinduzi ya Kodi Tanzania na somo kutoka IMF

Beng’i Issa aliongeza kuwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi kutasaidia kutoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo kukuza biashara zao, na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.