NEMC washinda tuzo uhabarishaji umma

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshinda tuzo ya ‘Stories of change’ kipengele cha taasisi ya serikali inayohabarisha umma kwa wakati na kuwajibika kwa wananchi katika utatuzi wa kero za kimazingira zinazowakabili kwa mwaka 2024.

Tuzo hiyo imetolewa na Jamii Forums katika jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dk Immaculate Semesi, Mkurugenzi Mkuu wa Jamii forums, Maxence Melo amesema baraza hilo limekuwa mstari wa mbele katika kujibu hoja za mitandao ya kijamii inayohusu masuala ya mazingira hali iliyoleta uwajibikaji na ushirikishwaji katika kusimamia na kuhifadhi mazingira katika jamii.

Amesema baraza limekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha umma hasa kwa habari za udhibiti wa sauti zilizozidi viwango, udhibiti taka hatarishi pamoja na umuhimu wa kutenganisha taka kutoka kwenye chanzo.

SOMA: Mabadiliko yaja kuipa mamlaka kamili NEMC

Awali ilielezwa kuwa taarifa zinazoleta mabadiliko kwa jamii kwenye mitandao kwa mwaka 2024 ziliwasilishwa 1800, hivyo kwa taaisis kupata tuzo ni uwajibikaji uliotukuka.

Hii ni mara ya nne kwa Jamii forums kuandaa tuzo za taarifa zinazoleta mabadiliko katika jamii zilizoandaliwa na taasisi mbalimbali pamoja na mashirika ya umma.

Habari Zifananazo

Back to top button