Netanyahu afanyiwa upasuaji wa tezi dume

ISRAEL: WAZIRI MKUU wa Israel, Benjamin Netanyahu amefanyiwa upasuaji wa tezi dume .

Upasuaji huo umekuja baada ya kugundulika alipata maambukizi  kwenye njia ya mkojo.

Kwa mujibu wa madaktari wanaoendelea kumtibu wamesema Waziri Mkuu Netanyahu anaendelea  vizuri na matibabu. SOMA: Kesi ya rushwa yamkabili Benjamin Netanyahu

Advertisement

Hatahivyo kufuatia  ugonjwa wa Netanyahu, Mshirika mkubwa wa Netanyahu ambaye ni Waziri wa Sheria Yariv Levin amepandishwa cheo kwa muda kushika nafasi ya waziri mkuu Netanyahu.

Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu anakabiliwa na matatizo ya afya lakini katika  taswira ya umma amejitahidi kuonekana kiongozi mwenye afya.