ISRAEL: WAZIRI Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amemfuta kazi waziri wake wa ulinzi, Yoav Gallant, na kusema amekosa imani naye.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa ofisini kwake, Netanyahu amesema hapo awali Gallant alikuwa muaminifu katika utendaji kazi hasa katika mipango ya kivita lakini sasa uaminifu huo haupo tena.
Amesema Gallant alifanya maamuzi ya kutoa taarifa bila ya kushirikisha baraza la mawaziri jambo ambalo limekwenda kinyume na utaratibu.
Hatahivyo, Yoav Gallant amesema ataendelea kulinda usalama wa taifa la Israel na utabaki kuwa jukumu la maisha yake.
Nafasi ya Yoav Gallant inatarajiwa kuzibwa na waziri wa mambo ya nje Israel Katzis.
Kambi za Upinzani nchini humo imekosoa hatua ya Netanyahu kumfuta kazi Gallant hasa katika kipindi hiki cha vita