Netanyahu apandishwa mahakamani

ISRAEL: WAZIRI MKUU wa Israel, Benjamin Netanyahu, amefikishwa mbele ya mahakama mjini Tel Aviv kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa.

Netanyahu aliwasili akiwa na timu yake ya mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha zawadi kutoka kwa marafiki mamilionea na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa matajiri wa vyombo vya habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji.

Hatahivyo, Waziri Mkuu Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. SOMA: Kesi ya rushwa yamkabili Benjamin Netanyahu

Netanyahu, mwenye umri wa miaka 75, ni waziri mkuu wa kwanza wa Israel kushtakiwa kwa uhalifu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button