Netanyahu: Tuko kwenye wakati mgumu

GAZA: WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema taifa lake linapitia kipindi kigumu baada ya wanajeshi saba kuuawa katika mapigano yanayoendelea mjini Gaza dhidi ya kundi la Hamas.

Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake wa X, Netanyahu alieleza masikitiko yake kwa vifo vya wanajeshi hao, akiwaita mashujaa waliopoteza maisha wakitekeleza operesheni ya kijeshi dhidi ya Hamas, pamoja na juhudi za kuwaokoa mateka walioko kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi la Israel, wanajeshi hao waliuawa baada ya gari walimokuwa wakisafiria kuripuliwa na bomu lililotegwa barabarani.

Tukio hilo limetokea huku kukiwa na ripoti kutoka kwa madaktari katika hospitali za Gaza zikieleza kuwa wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi raia wa Kipalestina waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula kusini mwa Gaza, na kusababisha vifo vya watu 44.

Mapigano hayo yanaingia mwezi wa 21 sasa, huku juhudi za upatanishi na misaada ya kibinadamu zikiendelea kukumbwa na changamoto. SOMA: Israel yasitisha huduma ya umeme Gaza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button