Ngorongoro Heroes kuzinduka leo?

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ inashuka dimbani leo katika mchezo wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) kanda ya CECAFA dhidi ya Djibouti.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa KMC uliopo Mwenge, Dar es Salaam.

SOMA: Vigezo ufunguzi, fainali Afcon 2027 vyatajwa

Advertisement

Katika mchezo wa kwanza Tanzania ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Kenya.

Ili kufufua matumaini Tanzania italazimika kushinda mchezo dhidi ya Djibouti ambayo katika mchezo wa kwanza ilifungwa mabao 3-1 na Sudan.

Mechi nyingine ya michuano hiyo leo itazikutanisha Sudan na Rwanda kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.