MCHEZO wa CAF Super Cup kati ya Al Ahly na Zamalek zote za Misri unafanyika leo kwenye uwanja wa Kingdom uliopo mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
SOMA: Al-Ahly klabu bora tuzo za CAF
Mchezo huo huzikutanisha bingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika, dhidi ya bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Al Ahly imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishinda Esperance Sportive de Tunis katika fainali Mei 25, 2024.
Nayo Zamalek imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikishobaada ya kuishinda RS Berkane katika fainali Mei 19, 2024.