‘Ni bajeti ya kutatua migogoro, umilikishaji ardhi’

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Dk Angeline Mabula amewasilisha liidhinishe kiasi cha Sh bilioni 171.4 ili kuiwezesha wizara yake kutekeleza mipango mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Miongoni mwa mambo sita ambayo Wizara imepanga kuyatekeleza katika mwaka ujao wa fedha, Dk Mabula ameliambia Bunge, Dodoma leo asubuhi kuwa ni kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi na kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi.

Waziri amesema mambo mengine yanayotarajiwa kutekelezwa ni kuwekeza zaidi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utunzaji wa, kumbukumbu, utoaji huduma na upatikanaji wa taarifa za ardhi pamoja na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji.

Wizara imepanga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia rahisi ya mawasiliano ya simu za mkononi; na kuimarisha mipaka ya kimataifa,” Waziri amelieleza Bunge.

Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara amemtaka Waziri kushughulikia migogo ya ardhi na fidia ya itolewe kulingana na thamani ya rasilimali.

Baadhi ya wabunge waliochangia hotuba hiyo baada ya Waitara wameitaka Wizara kupima ardhi yote ili kukabiliana na wingi wa migogoro ya ardhi hapa

Habari Zifananazo

Back to top button