Ni Valencia, ainyuka Qatar

MCHEZO wa kwanza wa ufunguzi wa michuano ya Fifa ya Kombe la Dunia umemalizika kwa wenyeji Qatar kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Ecuador.
Ni Enner Valencia aliyepeleka kilo kwa Waarabu hao baada ya kupachika magoli yote mawili.
Goli la kwanza amefunga dakika ya 15 na bao la pili dakika 30.

Kwa hapa nchini, mechi 24 za Kombe la Dunia zinarushwa moja kwa moja na Telivesheni ya Taifa (TBC) na mechi zote 64 zitarushwa kupitia TBC radio na TBC Online.

Katika ufunguzi wa michuano hiyo jana, Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano ya Umma, Nape Nnauye alishuhudia mtanange huo katika viwanja vya TBC Mikocheni.
Nape alisema “Nimepokea malamiko mengi kuwa TBC haipatikani kwenye ving’amuzi, nimeiagiza TCRA kushughulia suala hilo haraka.”
Senegal watarusha ndoano yao kesho Novemba 21,kuwakabili Uholanzi vijana wa Kocha Luis Van Gal

Senegal watashuka dimbani katika mchezo wao wa kwanza bila ya mshambuliaji wao tegemeo Sadio Manner ambae anauguza jeraha la mguu, alilopata wakati, akiichezea klabu yake ya Bayern Munich.
Kocha Aliou Cisse amesema, mshambuliaji huyo hahitaji upasuaji, na ana imani kuwa atapona haraka na kucheza mechi ya pili.
“Tutacheza mechi ya kwanza bila Sadio na tutashinda bila ya uwepo wake,” amesema Abdoulaye Sow kiongozi wa soka wa nchini hiyo.
Aidha, Uholanzi ambao wanacheza Kwa kushambukia dakika nyingi watashuka dimbani wakiwa na uhakika wa kiungo wao Frank De Jong.