DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Karimu Meshack amesema lengo kuu la bima ni kumrudisha mbima pale alipokuwepo awali.
Akiwa kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu ‘Sabasaba 2024’ leo Juni 07, 2024 jijini Dar es salaam, Meshack ametolea mfano, Bima ya Linda Mjengo inayokuhakikishia uhakika wa nyumba yako dhidi ya majanga kama vile moto, mafuriko.
“lengo la bima ni kumrudisha mbima pale alipokuwa awali kabla ya kupata majanga,kwa mfano mfano nyumba ya Milioni 100 ada yake ya bima laki 1 na 77,” amesema Meshack.
Kiongozi huyo pia hakusita kuzungumzia Bima Flexi inayowasaidia wafanyakazi yani badala ya kukata bima mtu mmoja mmoja badala yake Taasisi inasimama badala yao na huweza kujumuisha zaidi ya watu 50 ndani ya taasisi moja.
Katika msisitizo wake, Meshack ametoa wito kwa jamii kukata bima ya linda mjengo ili iweze kuwasaidia pale wanapopata majanga mbalimbali.