Nigeria yatangaza hali dharura ukosefu wa chakula

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu ametanga hali ya dharura ya uhaba na vyakula kupanda bei nchini humo. Shirika la Habari BBC rimeripoti.

Hata hivyo, imeelezwa miongoni mwa mikakati ya kuondokana na changamoto hiyo ni kutumia pesa zilizookolewa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta ili kutoa mbolea na nafaka kwa wakulima.

BBC imeripoti suala la ulinzi pia linapaswa kuongezwa kwa wakulima ambao wengi wao wameacha ardhi zao baada ya kuwa walengwa wa magenge huteka nyara na kupata pesa.

Mikakati hiyo inalenga kuzisaidia kaya maskini walau Dola 10 kila mwezi kwa muda wa miezi sita.

“Niwahakikishie Wanaigeria hakuna atakayeachwa nyuma katika mikakati hii.” amesema Tinubu ambaye aliingia madarakanu Mei.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa mwezi Januari ilikadiria kuwa Wanigeria milioni 25 walikuwa katika hatari kubwa ya uhaba wa chakula mwaka huu, ikimaanisha kuwa hawataweza kumudu chakula cha kutosha chenye lishe kila siku.

Wasiwasi kuhusu uhaba wa chakula umekuwa wa muda mrefu nchini Nigeria -nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambayo pia imekuwa ikipambana na ukosefu wa usalama kwa miaka kadhaa.

Zaidi ya wakulima 350 walitekwa nyara au kuuawa katika kipindi cha miezi 12 hadi Juni 2022 pekee, kulingana na tovuti ya ufuatiliaji wa usalama ya Nigeria.

Mengi ya mashambulizi haya yametokea kaskazini mwa nchi.

Lakini hatua mpya za usalama zitamaanisha wakulima wanaweza kurejea mashambani “bila kuogopa mashambulizi”, mshauri wa serikali Dele Alake alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button