NSSF yaongeza wanachama wapya 291,266 Kahama

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kahama umefanikiwa kuongeza wachamana wapya 291,266 kwa mwaka 2023/2024 na sasa inajipanga kuendelea kutoa huduma bora na zenye tija kwa wateja wao.

Haya yamebainishwa na Meneja wa Mfuko huo, Aisha Nyemba wakati akifungua Wiki ya Mteja kwa kuzungumza na kubadilisha mawazo na wanachama wao yenye kauli mbio”huduma bora muda wote”.

Advertisement

Amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2023/2024 mfuko ulikuwa na wanachama 1, 354, 985 na waajiri 43,430 na mwaka huo pia ilipata wanachama wapya 291,266 huku malengo yao yalikuwa kuandikisha wanachama 324,321 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

SOMA: NSSF yafikia Sh tril 8.5/- – HabariLeo

Aidha amesema mfuko umeboresha mfumo wa sekta isiyo rasmi mahususi kwa wanachama wote waliojiajiri, na umeandaa skimu maalum kwa wafanyakazi walio katika sekta rasmi ili kuweza kuchangia kwa hiari kupitia skimu hiyo.

Mkazi wa Ushetu, William Mtambo alisema,wawatembelee wakulima mara kwa mara na kuwaelimisha umuhimu wa mfuko huo na mafao ya baadaye ili kuwahamasisha kujiunga, wengi wanashindwa kuwa wanachama kwasababu ya kukosa elimu nasio vinginevyo.