NTC kutoa elimu lishe bora

CHUO cha Taifa cha Utalii (NTC) kimesema katika kuepuka kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kimejikita kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea upishi namna bora ya kuandaa vyakula vyenye lishe inayostahili.

Aidha kimesema kina mpango wa kutengenza mtaala ambao utazalisha wanafunzi wenye viwango vikubwa vya kimataifa ili kuweza kuwahudumia watalii kwa viwango vikubwa.

Meneja wa taaluma chuoni hapo, Mary Maduhu amesema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumza katika mashindano ya upishi kwa wanafunzi wa chuo hicho kwa kushirikisha wengine kutoka Zanzibar na chuo cha mafunzo Njuweni Kibaha, mkoani Pwani.

Mary amesema hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na hata saratani hivyo pia wanawafundisha wanafunzi wanaosomea mapsihi katika chuo kuhakikisha wanazingatia lishe anapoandaa chakula.

“Tunataka kurejea Eden, kwa kuwafundisha namna ya kupika kwa kuzingatia matunda mbogamboga, mbaazi kunde, nyama na samaki ili yule anayekula apate chenye kujenga mwili lakini pia katika hali ya usafi na usalama,” amesema Mary na kuongeza kuwa hali hiyo inasaidia mwanafunzi anapomaliza kuingia sokoni akiwa ameiva vya kutosha kuhudumia wateja.

Amesema kwa ufundisha lishe, itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi kwani awali walitumia zaidi jibini, sukari vijiko zaidi ya sita, mafuta lakini kwa sasa vinapikwa kwa uwiano unaolingana ili mradi ladha isipotee.

Amesema pia wanafundisha namna ya kudhibiti matumizi ya mafuta ambapo wanatumia ya mimea zaidi na kuongeza zaidi matumizi ya mbogamboga kwa wingi, mbegu kama mbaazi ambayo ina protini nyingi na matunda.

Kuhusu mashindano hayo amesema chuo kimeamua kufanya ushindani wa upishi kwa wanafunzi wao na wengine ilikudumisha ushirikiano na kuwajengea wanafunzi kujiamini haswa katika kipindi ambacho watalalii wanakuja kwa wingi nchini haswa baada ya filamu ya Royal Tour kuzinduliwa.

Amesema katika mashindano hayo waliwakuwa na majaji kutoka hotel kubwa nchini ili wakitoka hapo wawe wamefuzu kuwahudumia wateja.

“Rais Samia Suluhu Hassan amevutia watalii wengi kupitia filamu ya Royal Tour na kupitia chuo cha kitalii tunawafunisha ili watalii wanapofika nchini ambapo hukutana watoa huduma ikiwemo wa mapishi waweze kuhudumiwa kwa viwango vikubwa,” amesema na kuongeza kuwa chuo kimejikita kuboresha utalii.

Kuhusu uboreshwaji wa mitaala, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk Florian Mtei amesema wanataka kutengeneza mtaala ambao inayozalisha wanafunzi wenye viwango vikubwa vya kimataifa ili mtalii anapokuja akutane na chakula chenye viwango n ahata kwa waongoza watalii.

Amesema katika kutengeneza mitaala hiyo itasaidia watalii wanapotua nchini kufikia mikono ya watoa huduma mahiri ili asiweze kujuta kuhudumiwa na mhudumu aliyetoka katika chuo hicho.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button