KLABU ya soka ya Simba imetangaza kufikia mwisho wa mkataba na kiungo kiraka wake Erasto Edward Nyoni aliyehudumu klabuni hapo tangu mwaka 2017 hadi leo Juni 22, 2023 ambapo mkataba wake umefikia tamati.
Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 22, 2023 kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo na kusema hiyo ni sehemu ya uamuzi wa uongozi.
“Uongozi wa klabu unautangazia umma kuwa hatutaendelea kuwa na mchezaji wetu kiraka Erasto Nyoni baada ya mkataba wake kumalizika,” imesema taarifa hiyo.