Nyota Stars wajiapiza

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wamesema wako tayari kwa kuwakabili Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 kesho.

Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Honneir, Oudja, Morocco majira ya saa 6:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Taifa Stars inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi E, ikiwa na pointi sita katika michezo mitatu, Morocco ni kinara wa kundi hilo wakiwa na pointi 12.

“Tumefanya maandalizi yetu vizuri, naamini tutafanya vizuri, tunahitaji kushinda ili kujiweka sehemu nzuri zaidi kwenye kundi letu, Watanzania wanatutegemea kwahiyo hatuhitaji kuwaangusha,” alisema nahodha wa Taifa Stars, Simon Msuva.

Kwa upande wa beki wa kulia wa Simba na Taifa Stars, Shomari Kapombe alisema hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu ya ubora wa mpinzani.

“Mchezo utakuwa mgumu kwa sababu ya timu tunayoenda kucheza nayo, ina wachezaji wengi wanaocheza Ulaya, lakini utakuwa mgumu hata kwa upande wao,” alisema Kapombe.

Naye Selemani Mwalimu alimalizia kwa kuwataka mashabiki na wapenzi wa Taifa Stars wawaombee dua njema ili timu ipatae ushindi katika mchezo huo muhimu.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Tanzania, Morocco walipata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Novemba 21, 2023.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button