Nyumba za ibada zihimize msamaha

DAR ES SALAAM: MACHAFUKO yaliyolikumba taifa Oktoba 29, 2025 yamesababisha maumivu ya mwili na roho kwa Watanzania. Baadhi wamepoteza wapendwa wao, wengine wamejeruhiwa, wapo waliopoteza mali zao huku wengi wakibeba makovu ya kiakili na kihisia.

Hali hii imeacha mtikisiko mkubwa wa kijamii ambao umeleta athari kwa kila Mtanzania kwa namna tofauti wakiwemo waliosababisha machafuko hayo. Hiki ni kipindi ambacho kinahitaji zaidi uongozi wa kiroho unaojengwa juu ya upendo, busara, utulivu na kusamehe ili kusaidia kuponya roho zilizojeruhiwa na kurejesha amani ya kudumu.

Ni wajibu wa nyumba za ibada; makanisa, misikiti na taasisi nyingine za kidini kuchukua nafasi ya kuimarisha misingi ya imani, upendo na huruma.

Viongozi waendelee kuhubiri msamaha, maridhiano na kujenga uhusiano mwema miongoni mwa waumini na Watanzania kwa ujumla. Mafundisho yanayohimiza msamaha na kurekebisha mahusiano yaliyoharibika ni nguzo muhimu katika safari ya uponyaji wa taifa.

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuonesha njia ya msamaha pale alipotamka kuachiwa huru vijana waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka ya uhaini wakidaiwa kushiriki vurugu. Kutokana na madhara makubwa ambayo nchi imeyapata kutokana na vurugu hizo, isingekuwa rahisi kutoa msamaha huo kwa watu hao waliodaiwa kuhusika.

Lakini kutokana na kuangalia maslahi mapana ya nchi, Rais Samia ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu hakutanguliza hasira bali aliongozwa na busara na maandiko matakatifu yanayohimiza msamaha. Vinginevyo, asingeweza kuwaachia vijana hao badala yake, angeacha sheria ichukue mkondo wake.

Ni wajibu wa kila aliyepokea msamaha huo kuuthamini na kuukubali kama fursa ya kuanza upya. Hivyo, tunawahimiza vijana walioachiwa huru mahakamani kutambua kuwa msamaha waliopata si ruhusa ya kurudia makosa bali ni wito wa kuishi maisha ya nidhamu, uadilifu na kujenga amani.

Kuendelea kujihusisha na uhalifu, vurugu au uchochezi itakuwa ni kuvunja dhamira ya msamaha na kuhatarisha utulivu wa taifa. Kusamehewa ni heshima inayopaswa kulindwa kwa matendo chanya. Ni wajibu wa kila aliyepokea msamaha wa Rais Samia kuuthamini na kuukubali kama fursa ya kuanza upya.

Pamoja na juhudi za kisheria na za kijamii zinazolenga kuchunguza na kuelewa kiini cha vurugu, bado nchi inahitaji uponyaji wa kiroho na kujenga upya misingi ya uhusiano mwema.

Hili linawezekana tu iwapo jamii itaamua kusamehe, kuachilia yaliyopita na kutazama mbele kwa umoja bila kuendelea kufanya uchochezi au ‘kufukua makaburi’. Historia inaonesha kuwa mataifa yaliyokosa misingi ya kusameheana na kutatua mizozo kwa njia ya amani, hazijawahi kuwa na utulivu wa kudumu.

Msamaha ni tiba madhubuti kwa mwili na roho. Kwa kuwa kusamehe na kuachilia ni dhana ya kiroho, ndiyo maana tunahimiza viongozi wa dini kubeba ajenda hii na kuieneza kwa waumini.

Hata hivyo, tunapongeza madhehebu kadhaa ambayo tayari yameona umuhimu wa kuponya mioyo ya waumini kwa kuweka utaratibu maalumu wa maombi na toba. Kwa muktadha huo, tunawahimiza viongozi wa dini na madhehebu yote kushiriki kuiponya Tanzania na watu wake kwa mahubiri na matamko yanayohimiza amani, upendo na msamaha badala ya kuchochea chuki na hasira miongoni mwa Watanzania.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
    .
    Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button