DAR ES SALAAM; TAASISI ya Miriam Odemba Foundation (MOF), imewataka wadau wa maendeleo nchini kuchangia mkatati wa ukarabati na ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Mwendapole iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na HabariLEO, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Miriam Odemba amesema hali ya sasa ya vyoo katika shule hiyo haikidhi viwango katika suala la afya za wanafunzi.
“Tunawahimiza wafadhili na wadau wengine kuchangia katika jitihada zetu za kuboresha miundombinu ili kuhakikisha mazingira bora ya wanafunzi wetu kupata elimu,” amesema Miriam.
Isome pia:https://habarileo.co.tz/miriam-odemba-kujenga-vyoo-shule-ya-mwendapole/
Odemba amesema hatua hiyo ni muhimu katika kukuza afya na ustawi wa jamii ya Watanzania hivyo amewataka wadau wote wa maendeleo kuliangalia jambo hilo kwa jicho lingine.
Taasisi ya MOF imekuwa ikitoa msaada katika baadhi ya shule hasa kwa wanafunzi wa kike ili kuwahakikishia mazingira mazuri ya kusoma kwao.
Aidha Odemba amewataka wenye nia ya kufanikisha dhamira hiyo kuchangia kupitia namba 0749808073.