Oryx wapania kufungua vituo zaidi mikoani

Oryx wapania kufungua vituo zaidi mikoani

KAMPUNI ya nishati ya Oryx Tanzania, imesema imedhamiria  kufungua vituo zaidi vya mafuta kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta, ameeleza hayo leo wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa KFC- Thru na BAO Café katika kituo cha huduma cha Oryx Morocco jijini Dar es Salaam.

“Mahitaji ya bidhaa za nishati yanaongezeka mwaka hadi mwaka nchini Tanzania na Oryx Energies inapanua shughuli zake kwa kufungua vituo vipya katika miji ya Dodoma, Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar, ambapo tutaongeza wafanyakazi kusaidia vijana ambao hawana ajira,” alisema.

Advertisement

Kwa upande wake Vikram Desai, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, alielezea shauku yake kwa uzinduzi wa ushirikiano huo.

“Leo tunasherehekea uzinduzi wa ushirikiano huu mzuri na wa kimkakati kati ya Dough Works Limited na Oryx Energies Tanzania Limited.

“Pamoja na ufunguzi wa duka letu katika Kituo cha Oryx Morocco, tunaendelea kutimiza ahadi yetu ya kutoa chakula chenye ubora wa juu na kinachopatikana kwa urahisi nchini Tanzania.

KFC ni chapa ya kimataifa, yenye maduka 23,000 yaliyopo katika nchi zaidi ya 140 duniani kote.

“Tunayo furaha kusambaza huduma hii ya chakula yenye migahawa mashuhuri duniani kote na kutoa nafasi kwa watumiaji kupata huduma bora,” alisema.

/* */