Othman aanza safari ya kuimarisha chama

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ameanza ziara maalum ya siku nne kisiwani Pemba yenye lengo la kuimarisha mshikamano wa wanachama na kufufua ari ya kisiasa ndani ya chama hicho baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.

Ziara hiyo imeanza kwa shamrashamra kubwa katika eneo la Gombani, wilaya ya Chake Chake, ambako mamia ya wanachama na wafuasi walijitokeza kumpokea kwa shangwe. SOMA: Othman atwaa fomu ya urais Zanzibar

Kabla ya kuanza ziara hiyo Pemba, Othman alifanya mikutano kama hiyo kisiwani Unguja, akiwataka wananchi kudumisha umoja, amani na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya demokrasia na haki. “Ni wakati wa kila Mzanzibari kutambua wajibu wake katika kutetea haki. Hatutakubali kuburuzwa wala kudharauliwa,” alisema mbele ya umati uliofurika.

Katika ziara hiyo, Othman anatarajiwa kutembelea mikoa yote minne ya kichama kisiwani Pemba na kufanya vikao na viongozi, wanachama na wananchi kusikiliza changamoto zao na kujadili mustakabali wa Zanzibar kisiasa. Ni ziara yake ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliompa ushindi Dk. Hussein Ali Mwinyi wa CCM kwa asilimia 74.8, huku Othman akipata asilimia 23.3.

 

Habari Zifananazo

6 Comments

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

      .

      This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button