Pamba Jiji kuzindukia Tanzanite Kwaraa leo?

Sehemu ya wachezaji wa Fountain Gate wakisamilia mashabiki katika moja ya michezo ya timu hiyo.

FOUNTAIN Gate leo ni wenyeji wa Pamba Jiji katika mchezo pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoa wa Manyara.

Ikiwa imecheza mechi raundi 10, Fountain Gate inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu ikijikusanyia pointi 17 wakati Pamba Jiji ni ya 15 ikiwa na pointi 5 kwa michezo 10 pia.

SOMA: Fountain Gate kuendeleza ubabe Ligi Kuu leo?

Advertisement

Katika mechi pekee ya ligi hiyo iliyofanyika Novemba 4, Dodoma Jiji imepoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo tisa wakati Ken Gold ni ya mwisho ikiwa na pointi tano baada ya michezo 11.