Papa Francis kukutana na viongozi wa dini
INDONESIA : KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis anatazamiwa leo kusisitiza utangamano wa kidini, atakapokutana na viongozi wa dini nyingine sita za Indonesia.
Papa Francis anatarajiwa kutia saini tamko la pamoja na Imamu mkuu wa msikiti huo, linalohusu ulinzi wa mazingira na kudunisha utu wa binadamu unaosababishwa na migogoro, kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Indonesia.
SOMA : Papa Francis ahimiza masikizano na kuishi kwa kuvumiliana nchini Indonesia
Katika ziara yake hiyo, Papa Francis ataendesha misa itakayohudhuriwa na maelfu ya watu katika uwanja wa mpira wa miguu katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta na kuwahimiza waumini wa dini zote wawe wastahimilivu wa kidini.