MICHEZO ya Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea leo baada ya kusimama kupisha mechi za kimataifa ambapo viwanja vitatu vitawaka moto.
Coastal Union iliyohamia Arusha itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Coastal ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 7 wakati Dodoma Jiji ni ya 6 ikiwa na pointi 9.
SOMA: Vibonde kuzinduka Ligi Kuu leo?
Katika mtanange mwingine Azam ni wageni wa maafande wa Tanzania Prisons kwenye uwanja Sokoine jijini Mbeya.
Prisons ni ya 11 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 6 wakati Azam inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 7.
Maafande wa JKT Tanzania watakuwa uwanja wa nyumbani wa Maj Gen Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam kuikaribisha Tabora United.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 6 wakati Tabora United ni ya 9 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 7.