LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa Dar es Salaam, Mbeya na Lindi ikihusisha timu tatu zinazoshika nafasi a mwisho katika msimamo wa ligi.
Ken Gold inaikaribisha Tabora kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Yanga katika mchezo uliopita.
SOMA: Kagera vs KenGold: Kipute cha waliohoi Ligi Kuu
Klabu hiyo ya Mbeya iliyopanda Ligi Kuu ndio inayoshika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo huku Tabora United ikiwa ya 6 ikikusanya pointi 7 baada ya michezo 5.
Kwenye uwanja wa Azam Complex , Dar es Salaam klabu nyingine iliyohoi, Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Pamba Jiji.
Coastal ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 5 wakati Pamba Jiji inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 4.
Tanzania Prisons imesafiri hadi Ruangwa mkoani Lindi kuifuata Namungo ambayo nayo inasuasua katika msimamo wa ligi, mchezo ukifanyika uwanja wa Majaliwa.
Prisons ipo nafasi ya 11 ikiwa na ponti 4 baad ya michezo 4 wakati Namungo inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 3.