Pauni mil 148 kumhamisha Haaland kwenda Barcelona

TETESI za usajili zinasema nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland ameamua anataka kujiunga na klabu ya Barcelona badala ya Real Madrid na anapanga kuhamia mwaka 2026.
Barcelona sasa inafanyia kazi mpango wa kukusanya pauni milioni 148.2 kuhuisha kipengele cha kuachiwa mchezaji huyo Man City. (El Nacional – Spain)
Anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Haaland Man City ni mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike.
Mkurugenzi wa michezo anayetarajiwa kujiunga na Man City, Hugo Viana amefungua mazungumzo ili kuzishinda Arsenal, Chelsea na Man Utd kumsajili mfaransa huyo. (BILD – Germany)
Wakati huo huo Barcelona inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Porto, Samu Aghehowa kama mbadala wa Robert Lewandowski, ambaye umri wake unaendelea kumtupa mkono kwenye soka la ushindani.
Pia Man United inasaka saini ya kinda huyo wa kihispania. (Sempre Barca – Spain)
Napoli imeibuka kuwa sehemu sahihi kwa fowadi wa Liverpool, Darwin Nunez, ambaye ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo kwa bei inayofaa majira haya ya kiangazi. (Corriere dello Sport – Italy)
Arsenal inakaribia kushinda mbio za kumsajili golikipa wa Espanyol, Joan Garcia. (The Independent)