PIC: Tumeridhika mradi wa SGR Tabora -Kigoma

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC) imesema kuwa utekelezaji wa mradi wa Reli ya Kisasa wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma una faida kubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwa shehena kubwa kusafirishwa kwenda nchi za ukanda wa maziwa makuu hivyo kuongeza pato la serikali kwa kiasi kikubwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Augustino Vuma Holle amesema hayo akiongoza kamati hiyo kutembelea utekelezaji wa mradi huo kipande cha Tabora hadi Kigoma Lot 6 ambapo wamefurahishwa mradi kutekelezwa na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutachochea serikali kukusanya mapato makubwa katika usafirishaji wa mizigo na abiria kwa haraka.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TRC) Ally Karavina akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya bunge ya uwekezaji mitaji ya umma ilipotembelea mradi wa SGR Tabora hadi Kigoma

Vuma Holle amesema wanaridhishwa kuanza kwa mradi huo kwani mradi huo unagusa maisha ya wananchi wa mikoa ya magharibi moja kwa moja lakini pia biashara za wananchi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu ambapo wamekuwa wakitumia bandari ya Kigoma kusafirisha bidhaa zao hivyo reli hiyo itarahisisha ufanyaji wa biashara kwa kiwango kikubwa.

“Tumeridhishwa na hatua ambayo mradi umeanza ukiwa umefikia asilimia saba ambapo serikali imetoa kiasi cha shilingi trilioni tofauti na maneno ya watu kwamba mradi huo umetelekezwa na sisi tutaendelea kupiga kelele kuhakikisha fedha zinatoka na mradi unakamilika,” Mwenyekiti wa PIC amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRL Ally Karavina (katikati) akiwaongoza wajumbe wa kamati ya Bunge ya PIC kutembelea mradi wa SGR Tabora hadi Kigoma

Akizungumza mbele ya kamati hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli nchini (TRC), Ally Karavina amesema kuwa wanaendelea na utekelezaji wa mradi huo kwa kilometa 2000 kwa maeneo yote kama ambavvyo wamepokea maelekezo ya Rais Samia kuhakikisha utekelezaji unafanyika.

Karavina amesema kuwa reli hiyo ya kisasa kwenda Kigoma ina umuhimu mkubwa katika kuisadia Bandari ya Dar s Salaam kuharakisha utoaji mizigo kwenda nchi za ukanda wa maziwa makuu ambapo kwa sasa kumekuwa na malalamiko kidogo kwa wateja hivyo kukamilika kwa reli hiyo kutainua utendaji wa shirika hilo lakini kutekeleza mkakati wa serikali wa kuinua uchumi wa nchii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button