DAR ES SALAAM – Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, amesaini kitabu cha Maombolezo na kukimfariji mjane wa marehemu Dk. Faustine Ndugulile, Dk. Magdalena Lyimo na Mama mzazi wa marehemu, Bi. Martha Ndugulile wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Kigamboni, Jijini Dar es salaam leo Novemba 29.
Dk. Ndugulile alifariki dunia Novemba 27 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.