DAR ES SALAAM :BAADHI ya waombolezaji wakiwemo wabunge wakiwa Uwanja Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea mwili wa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani ((WHO) Kanda ya Afrika, hayati Dk Faustine Ndugulile unaotarajiwa kuwasili nchini leo.
Dk Ndugulile alifariki dunia usiku wa kumkia juzi nchini India akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge la Tanzania, mwili wa kiongozi huyo unatarajiwa kufikishwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) mchana wa leo.