PICHA| Marehemu King Kikii anaagwa Leaders

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro

DAR ES SALAAM – Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official amewasili katika uwanja wa Leaders jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga mwili wa nguli wa muziki wa dansi nchini Marehemu Kikumbi Mpango Mwanza (King Kikii) aliyefariki dunia Novemba 15, 2024.

Marehemu King Kikii  atazikwa leo Novemba 18, 2024 katika makaburi ya Kinondoni.

Advertisement